Messi ashangaa Argentina kufungwa na Morocco Olympic 2024
Sisti Herman
July 25, 2024
Share :
Baada ya mchezo wa kwanza wa Olympic kundi B kati ya Argentina na Morocco ambapo Morocco walishinda 2-1, nahodha wa taifa hilo Lionel Messi alichapisha ujumbe wa kushangazwa kwenye mitandao yake ya kijamii.
Messi kupitia Insta Story yake aliandika "Insolito" akimaanisha "Siamini" baada ya mwamuzi wa mchezo huo kukataa lililokuwa goli la kusawazisha la Argenina dakika ya mwisho ya mchezo huku msaada ya picha za marejeo ukionyesha kuwa mchezaji wa Argentina Cristian Medina aliotea kabla ya kufunga.
Magoli mengine ya mchezo hupo yalifungwa na Sofiane Rahimi aliyefunga mawili kwa upande wa Morocco na Giuliano Simeone kwa upande wa Argentina.
Argentina na Uruguay wanaburuza mkia wa kundi B wakiwa na alama sifuri huku Morocco na Iraq wakiongoza wakiwa na alama 3.
Michuano ya Olympic hujumuisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 23 huku wakiruhusu wachezaji watatu wazoefu wenye umri zaidi ya huo.