pmbet

Messi atinga saa ya Bilioni 2.3

Sisti Herman

August 1, 2025
Share :

 

Staa wa Inter Miami na Argentina, Lionel Messi ameonekana akiwa amevaa saa ya kifahari ya rangi ya waridi aina ya Rolex Daytona “Barbie”, yenye thamani ya takribani Pauni 700,000 (zaidi ya Sh2.3 bilioni).

Kiasi hicho cha fedha kinaweza kununua magari ya kifahari aina ya Toyota Land Cruiser 300 matano ambayo bei yake ni kuanzia Sh 450 milioni na Sh 520 milioni.

Nyota huyo wa Inter Miami alionekana na saa hiyo ya bei ghali Jumamosi usiku wakati timu yake ikitoka suluhu dhidi ya FC Cincinnati.

Messi (38), hakuwa uwanjani kwani alikuwa anatumikia adhabu ya kufungiwa kucheza mechi moja.

Mshindi huyo mara nane wa tuzo ya Ballon d’Or alikaa jukwaani pamoja na mtoto wake Thiago (12), akiwa amevalia shati jeupe na kaptula ya beige lakini kiliteka shoo kilikuwa ni saa yake ya ajabu ya Rolex Barbie.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet