pmbet

Messi atoa msaada wa Milioni 244 Madrid.

Joyce Shedrack

August 5, 2026
Share :

Nyota wa Inter Miami na nahodha wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi, ameonyesha tena moyo wake wa kusaidia jamii baada ya kutoa mchango wa takribani euro 80,000 sawa na Milioni 244 za Kitanzania kwa ajili ya kusaidia juhudi za ujenzi upya katika eneo la Sierra Oeste, mkoani Madrid Nchini Hispania.

Lionel Messi: Biography, Soccer Player, Inter Miami, Argentina, World Cup

Eneo hilo la vijijini liliharibiwa vibaya na moto mkubwa wa misitu ulioteketeza karibu ekari 75,000, ukiharibu mazingira ya asili, miundombinu muhimu na kuwaacha wakazi wengi bila makazi.

 

Mchango huo wa Messi unalenga kusaidia kurejesha hali ya kawaida katika eneo hilo baada ya janga hilo la mazingira.

Rais wa Mkoa wa Madrid, Isabel Díaz Ayuso, alithibitisha taarifa hizo kupitia mtandao wa X, akimshukuru nyota huyo wa zamani wa Barcelona kwa ukarimu wake.

 

“Lionel Messi ametoa euro 80,000 kwa ajili ya ujenzi upya wa Sierra Oeste ya Madrid. Ninataka kumshukuru na kumwambia kuwa sisi watu wa Madrid tunatarajia kumpokea hivi karibuni na kumpigia makofi anayostahili,” aliandika Ayuso.

 

Hatua hiyo imepokelewa kwa pongezi nyingi, huku ikiongeza sifa za Messi kama mmoja wa wanamichezo wanaotumia mafanikio yao kusaidia jamii wakati wa majanga.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet