Messi hukustahili Tuzo Bora ya FIFA - Matthäus
Eric Buyanza
January 20, 2024
Share :
Lothar Matthäus, mshindi wa zamani wa Ballon d’Or, amesema Lionel Messi nahodha wa Argentina hakustahili Tuzo Bora ya FIFA kwa 2023.
Akiongea na kituo cha Sky Deutschland, Matthaus amesisitiza kwamba Messi hakustahili na kwamba Erling Haaland wa Manchester City ndiye aliyepaswa kushinda tuzo hiyo.
Messi hivi majuzi alishinda Tuzo Bora ya FIFA akimpiku Haaland na Kylian Mbappe.
"Hawezi kuwa mshindi wakati huu. Nadhani alikuwa mwanasoka bora zaidi wa miaka 20 iliyopita, lakini amekuwa Paris na Miami, ambako sasa anatengeneza kelele, na hajashinda taji lolote kubwa,” Matthaus alisema.
"Ukiangalia mafanikio makubwa, hakuna njia kuipita Manchester City wakati wa kuchagua mchezaji bora, Erling Haaland alishinda mataji muhimu zaidi akiwa na Man City. Kiwango chake kilikuwa cha kuvutia."
“Hivyo yanapaswa kuwepo maamuzi makini unapochagua mchezaji bora na hiyo ilikuwa Haaland.”