pmbet

Messi kucheza timu ya Taifa chini ya miaka 23 Olympic 2024

Sisti Herman

February 14, 2024
Share :

Kocha wa timu ya Taifa ya Argentina chini ya miaka 23 Javier Mascherano amemfungulia milango nyota wa klabu ya Inter Miami na timu ya Taifa ya Argentina, Leonel Messi ambaye anatajwa kujumuika na kikosi cha timu ya Taifa ya Argentina U23 kwenye fainali za Olympic ambazo zitafanyika Paris nchini Ufaransa.

 

“Kila mtu anafahamu uhusiano wangu na Leo [Messi], na urafiki tulionao, Mchezaji kama yeye milango ipo wazi kwenda na sisi [Olympic], sasa itabakia kwake na uamzi wake”, alisema Mascherano ambaye pia alicheza na Messi Barcelona na Argentina.

 

Argentina imefuzu kwenye michuano ya Olympic 2024 baada ya kuwaondoa mabingwa wa michuano hiyo timu ya Taifa ya Brazil kwenye mchezo wa kusaka tiketi ya kishiriki michuano hiyo.

 

Nahodha wa timu ya Taifa ya Argentina U23 Thiago Almada amesema anatumaini Messi atajiunga na kikosi hicho kwenye majira ya joto mwaka huu na atampatia kitambaa cha unahodha.

 

“Natumaini Messi atakuwepo kwenye michezo ya Olympic,na itakuwa ndoto, Kama Messi ataungana na sisi basi nitampa kitambaa cha unahodha”, Alisema Thiago.

 

Mara ya mwisho kwa timu ya wanaume ya Argentina kushinda michuano hiyo ilikuwa mwaka 2008 iliyofanyika nchini Beijing na Messi alikuwa sehemu ya kikosi hicho.

 

Kwenye michuano ya Olympic licha ya kujumuisha wachezaji wenye umri mdogo lakini pia yanatoa nafasi chache kwa wachezaji wenye umri mkubwa kujiunga na vikosi vya timu za Taifa zilizofuzu ili kuongeza chachu ya ushindani kwa vijana.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet