Messi na Lamine Yamal vinara wa chenga Kombe la Dunia.
Joyce Shedrack
July 18, 2026
Share :
Lionel Messi na Lamine Yamal ndio wachezaji wawili pekee waliofanikiwa kukamilisha chenga na kukokota mpira'dribbling' zaidi ya 20 katika Kombe la Dunia 2026 wakionyesha ubora wao wa kipekee katika kuwapita mabeki.
Nahodha wa Argentina, Lionel Messi anaongoza orodha hiyo kwa kukamilisha chenga 25 huku nyota wa Hispania na Barcelona Lamine Yamal akifuatia kwa chenga 22.
Takwimu hizo zinaonyesha mchango mkubwa wa wachezaji hao wawili katika mafanikio ya timu zao kufika hatua ya fainali, ambapo wanatarajiwa kukutana katika pambano la kuwania taji la dunia siku ya kesho.





