pmbet

Messi na Ronaldo kuvaana kama wamiliki wa vilabu nchini Hispania

Eric Buyanza

October 3, 2026
Share :

Moja ya ushindani mkubwa na wa kihistoria katika ulimwengu wa soka unatarajiwa kuhamia rasmi kwenye vyumba vya bodi za wakurugenzi na majukwaani nchini Hispania, kufuatia hatua ya magwiji Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kumiliki vilabu vinavyoshiriki ligi moja ya daraja la pili (LaLiga 2).

 

Hali hii inatengeneza dabi ya kipekee ambapo klabu ya UD Almería inayohusishwa na Ronaldo na CD Eldense inayomilikiwa na Messi, zitakutana uso kwa uso kwa mara ya kwanza mnamo Mei 2, 2027.

 

Ushindani huu wa nje ya uwanja ulianza mnamo Februari 2026, pale mshambuliaji wa Al-Nassr, Cristiano Ronaldo, aliponunua rasmi hisa za umiliki wa asilimia 25 (25% stake) katika klabu ya UD Almería kupitia kampuni yake ya CR7 Sports Investments.

 

Katika kile kinachoonekana kama kujibu mapigo, staa wa Inter Miami, Lionel Messi, amekamilisha ununuzi wa umiliki wa asilimia 100 (100% owner) wa klabu ya CD Eldense. Ununuzi huo wa Eldense—klabu iliyoanzishwa mwaka 1921 inayotumia rangi za kufanana na klabu ya zamani ya Messi, Barcelona.

 

Ratiba ya ligi ya LaLiga 2 msimu huu imepanga mchezo huo wa kihistoria katika mzunguko wa lala-salama (Wiki ya 37). Mashabiki na wachambuzi wa soka duniani kote tayari wameanza kuonyesha shauku kubwa ya kushuhudia dabi hii, huku kukiwa na uwezekano mkubwa wa timu zote mbili kuwa kwenye mapambano makali ya kupanda daraja kwenda Ligi Kuu (LaLiga) zikichangiwa na uwepo wa Messi na Ronaldo kwenye majukwaa ya VIP.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet