Messi ndiye mchezaji mwenye asisti nyingi ktk historia ya kombe la dunia
Eric Buyanza
July 4, 2026
Share :
HISTORIA
Ni rasmi sasa kuwa Lionel Messi ndiye mchezaji mwenye pasi za mabao (assists) nyingi zaidi katika historia ya Kombe la Dunia, akiwa amefikisha jumla ya assists 9.
Kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia 2026, Messi alikuwa amelingana na aliyekuwa nguli wa soka Diego Maradona wakiwa na pasi 8 kila mmoja. Katika mechi ya hatua ya 32 bora ya Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Cape Verde, Messi alipiga mpira wa kona uliosababisha bao la ushindi. Pasi hiyo ilimfanya rasmi kufikisha assists 9 na kushika usukani kama mfalme wa pasi za mabao katika historia ya kombe la dunia.






