Messi: Real Madrid ni timu bora duniani
Sisti Herman
June 7, 2024
Share :
Akiwa kwenye mahojiano na kituo cha televisheni maarufu nchini Argentina cha iNFOBAE, mchezaji bora wa dunia na mshindi wa tuzo ya Ballon D'or mara 7 Lionel Messi amesema kuwa klabu ya Real Madrid ndiyo timu bora zaidi kwasasa duniani licha ya kuwa timu hasimu na klabu ya maisha yake Barcelona.
"Timu bora zaidi ni Real Madrid, wameshinda ligi ya Mabingwa, ukiongoelea kuhusu matokeo mazuri ni Real Madrid ila Man City inacheza vizuri" alisema Messi.
Messi amefanya mahojiano hayo na mwanahabari maarufu Alvarez Pollo akiwa kwenye kambi ya timu ya Taifa inayojiandaa na michuano ya Copa America.