pmbet

Messi wa Timu ya Wanawake ya Barcelona aacha vilio kwa mashabiki.

Joyce Shedrack

May 27, 2026
Share :

Mshindi wa Ballon d’Or mara mbili, Alexia Putellas raia wa Hispania ameacha vilio na majonzi kwa mashabiki wa FC Barcelona baada ya kutangaza rasmi kuondoka klabuni hapo kufuatia utumishi wa misimu 14 katika klabu ya Wanawake ya Barcelona.

 

Klabu ya Barcelona ilithibitisha usiku wa jana habari iliyowashtua mashabiki wa soka huku wakiweka wazi siku ya leo nyota huyo wa ligi ya Wanawake aliyepewa jina la Messi wa kike ataagwa rasmi katika hafla itakayofanyika kwenye uwanja wa Camp Nou.

L'Espagnole Alexia Putellas remporte le Ballon d'Or pour la deuxième année  consécutive - Le Temps

Putellas mwenye umri wa miaka 32, siku ya Jumamosi alisaidia Barcelona kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya nne katika misimu sita na hakukuwa na tangazo la haraka kuhusu hatma yake huku kukiwa na tetesi kuwa anaweza kujiunga na London City Lionesses.

 

Nguli huyo ameichezea Barcelona mechi 507  tangu alipowasili akiwa na umri wa miaka 18 mwaka 2012 kutoka Levante UD Femenino akifunga mabao 232 kwa Barcelona na kuweka rekodi ya klabu huku akishinda mataji 38, yakiwemo Ligi ya Mabingwa Ulaya mara nne na mataji 10 ya ligi ya Hispania pamoja na Kombe la Dunia la Wanawake mwaka 2023.

 

Alikuwa mchezaji bora wa Barcelona iliposhinda Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza mwaka 2021 na alishinda tuzo za Ballon d’Or mfululizo mwaka 2021 na 2022. 

 

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet