Mexime ajiunga na walima mpunga wa Mbarali
Eric Buyanza
December 28, 2023
Share :
Siku 5 baada ya kuachana na Kagera Sugar, Kocha Mecky Mexime amejiunga na walima mpunga wa mbarali klabu ya Ihefu ya jijini Mbeya na kumfanya kuwa kocha wa 4 kuiongoza Ihefu msimu huu.
Makocha watatu tayari wamepita Ihefu msimu huu ambao ni John Simkoko (aliyeomba kupumzika), mwezi Septemba, Zuberi Katwila aliyetimuliwa baada ya kuwa na matokeo mabaya na nafasi yake ikachukuliwa na moses Basena ambaye nae hakudumu.