MFALME WA MISRI: Mo Salah avunja rekodi iliyodumu miaka 20
Eric Buyanza
November 14, 2026
Share :

Nahodha wa timu ya taifa ya Misri, Mohamed Salah, ameandika historia mpya katika soka la nchi hiyo baada ya kufikisha mabao 70 na kuwa mfungaji bora wa muda wote wa kikosi hicho ("The Pharaohs").
Salah, ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Trabzonspor ya Uturuki, alivunja rekodi hiyo usiku wa kuamkia leo Jumamosi wakati Misri ilipoiadhibu Malawi mabao 5-0 katika mchezo wa kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027) uliopigwa kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Cairo.
Rekodi hiyo kwa muda wa miaka 20 ilikuwa ikishikiliwa na gwiji wa zamani wa nchi hiyo, Hossam Hassan, akiwa na mabao 69.
Kwa kufikisha mabao 70 katika mechi 123 tangu aanze kuitumikia timu ya taifa mwaka 2011, Salah sasa anashika nafasi ya tatu katika orodha ya wafungaji bora wa muda wote wa timu za taifa barani Afrika, akimfuatia gwiji wa Malawi, Kinnah Phiri (mabao 71) na kinara wa muda wote kutoka Zambia, Godfrey Chitalu (mabao 79).





