pmbet

Mfanyabiashara Chivayo afariki dunia kwa ajali ya Helicopter

Sisti Herman

October 1, 2026
Share :

 

Mfanyabiashara wa Zimbabwe, Wicknell Chivayo, na mkewe, Lucy “Lulu” Muteke, walifariki dunia Jumatano jioni baada ya helikopta kuanguka katika eneo la vijijini la Marondera, mashariki mwa Harare.

Jeshi la Polisi la Zimbabwe lilithibitisha ajali hiyo ya chombo cha anga, iliyotokea majira ya saa 11 jioni, likisema kuwa chombo hicho kilikuwa na watu sita ndani. Polisi walisema maelezo zaidi yatatolewa kadiri uchunguzi unavyoendelea.

Baadaye, msemaji wa serikali Nick Mangwana alithibitisha kuwa hakuna aliyenusurika; watu saba walikuwa ndani ya helikopta hiyo, akiwemo Chivayo, abiria wengine wanne na marubani wawili.

Mamlaka bado hazijabaini chanzo cha ajali hiyo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet