Mfumo wa kusambaza dawa vijijini kwa 'Drone' wakamilika
Eric Buyanza
February 6, 2024
Share :
Serikali imesema tayari imekamilisha mfumo ambao unahifadhi taarifa zote za vituo kuanzia ngazi ya Zahanati hadi Taifa, ambao utasaidia kupata taarifa za kijiografia (Geo coordinates) za vituo vyote nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, wakati akijibu swali kwa niaba ya Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu, lililoulizwa na Mbunge wa Kilindi Mhe.Omari Mohamed Kigua, aliyeuliza “Je, ni lini Serikali itatumia Drones kusambaza Dawa katika Zahanati zetu Vijijini?".
Dkt. Mollel, amesema taarifa zitakazohifadhiwa kwenye mfumo huo zitasaidia kufanya majaribio ya usafirishaji wa dawa kwa kutumia ndege zisizo na rubani (drones), pamoja na kulinganisha gharama za usafirishaji kwa njia hiyo na ile ya magari, ili maamuzi sahihi yafanyike.
ITV