pmbet

Mgema 'Pombe ya Mnazi' anayemiliki Ndinga na Ghorofa!

Eric Buyanza

December 21, 2023
Share :

Biashara ya pombe ya mnazi imekuwa ikidharaulika sana kwa hapa Tanzania, lakini kwa wenzetu Nigeria ni biashara kubwa na pombe yenye heshima haswa watu wanaoheshimu utamaduni.
 

Kwa hapa kwetu Bongo hata wanywaji wa pombe hiyo pia sio watu wanaoheshimika.
 

Taarifa ikufikie kuwa huko Nigeria jamaa mmoja kwa jina la Utobo ambaye ni mgema pombe ya mnazi (namaanisha yule anayepanda kwenye mnazi kutega pombe) anamiliki gari aina ya Mercedez Benz na hivi tunavyoongea anamalizia ujenzi wa nyumba yake ya ghorofa la kifahari.
 

Utobo mwenye miaka 37 ambaye ghorofa analomalizia ni nyumba yake ya pili anasema katika masaa 24 tuliyopewa na mwenyezi mungu....yeye anatumia masaa 19 akiwa juu ya miti kugema pombe.
 

Kwa mujibu wa Utobo anapanda juu ya miti 53 mara tatu kwa siku na anapata madumu 24 ya pombe mpaka muda anaenda kupumzika.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet