Mgomo wa wafanya biashara Kariakoo, maduka yote yafungwa
Sisti Herman
June 24, 2024
Share :
Baada ya vipeperushi kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kuwepo kwa mgomo wa wafanyabiashara Soko la Kariakoo, leo mpaka kufikia saa 3 asubuhi maduka mengi bado hayajafunguliwa.
Leo Jumatatu, Juni 24, 2024, wafanyabiashara katika eneo hilo wakiwa wamekaa nje, huku maduka yao yakiwa yamefungwa.
Biashara pekee inayoendelea ni ile inayofanywa na wafanyabiashara ndogondogo 'machinga' katika mitaa mbalimbali sokoni hapo.
Wakati vipeperushi vikisambaa kwenye mitandao ya kijamii vikieleza kuhusu mgomo wa wafanyabiasha Kariakoo kuanzia leo Jumatatu, uongozi wao uliwataka kuwa watulivu, ukisema tamko litatolewa.