pmbet

Mgomo wa wafanyabiashara washika kasi nje ya Dar es Salaam.

Eric Buyanza

June 26, 2024
Share :

Ikiwa ni siku mbili tangu wafanyabiashara soko la Kariakoo kuanza mgomo, Wafanyabishara masoko mengine nje ya Dar es Salaam nao wameanza kufunga maduka huku wakisisitiza hawatafungua maduka mpaka wasikilizwe hoja zao. 

Siku ya leo wafanyabiashara mbalimbali wamefunga maeneo yao ya biashara huku wakisema kuwa ni kuunga mkono mgomo wa wafanyabiashara unaoendelea katika maeneo ya soko la Kariakoo jijini Dar es salaam, Mbeya, Dodoma, na Mwanza ambao unalenga kuishikikiza Serikali iyafanyie kazi madai yao 14 likiwemo suala la kamata kamata zoezi ambalo limekuwa likiendeshwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pamoja na kukithiri kwa utozwaji wa kodi.

Maeneo ambayo siku ya leo wamefunga maduka ni Arusha na Mkoa wa Kigoma.

Hata hivyo,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekuta na uongozi wa jumuiya ya wafanyabiashara leo Juni 26,2024 kwa ajili ya kuzungumza nao na kutafuta utatuzi wa kile kinachoendelea.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet