pmbet

Mgonjwa afariki kwa kujinyonga na shuka akiwa wodini

Eric Buyanza

February 6, 2024
Share :

Batromeo Bernad, Mkazi wa Mtaa wa Ndege Wengi, uliopo mkoani Morogoro, amefariki dunia kwa kujinyonga na shuka akiwa wodini katika hospitali ya Rufaa ya Morogoro, alipokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu.
 

Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu, wamedai kuwa walimfikisha Batromeo Hospitalini hapo, wiki mbili zilizopita akisumbuliwa tatizo la afya ya akili.
 

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama, ambaye amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akibainisha bado wanaendelea na uchunguzi.
ITV

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet