Mhalifu aomba ushauri wa kuwekeza pesa, kutoka kwa aliyempora
Eric Buyanza
May 24, 2024
Share :
Mwaka 1996 jambazi, mtekaji na mhalifu maarufu wa kichina, Cheung Tze-Keung akiwa Hong Kong alimteka nyara mtoto wa Bilionea wa nchi hiyo (kipindi hicho) aliyefahamika kwa jina la Li Ka-shing na kuchukua fidia ya pesa za thamani ya dola za HongKong milioni 130 na kisha akamuachia mtoto huyo.
Kilichowashangaza wengi ni kitendo cha mhalifu huyo baadae kumpigia simu Bilionea na kumuomba amsaidie ushauri wa jinsi ya kuwekeza pesa hizo ili ziweze kumzalishia faida.
Bilionea anasema anakumbuka alimwambia jambazi huyo kwamba alikuwa amechukua pesa za kutosha kutumia maisha yake yote, na ni bora akasafiri na kwenda kumalizia maisha yake mbali kabisa.
Cheung Tze-keung alikuwa jambazi maarufu wa Hong Kong aliyejulikana pia kwa jina la "Big Spender", alikuwa mteka nyara, jambazi, mlanguzi wa silaha na alikuwa akitafutwa kesi nyingi za mauaji.