pmbet

Mhitimu Chuo Kikuu ajinyonga baada ya kuomba kazi 500 bila mafanikio

Eric Buyanza

January 12, 2024
Share :

Vera Omondi, mhitimu wa Chuo Kikuu cha Masinde Muliro nchini Kenya kwa 2019, amejiua kwa kujinyonga baada ya kushindwa kupata kazi miaka mitano baada ya kumaliza masomo yake.
 

Inadaiwa kwamba mwanadada huyo kabla ya kuchukua hatua hiyo, alikuwa amelalamika kwamba kati ya maombi 500 aliyotuma kutafuta ajira, hakuna kazi hata moja aliyoitwa.
 

Mwili wa Vera uligunduliwa na mama yake mzazi ukiwa unaning’inia bafuni nyumbani kwao katika kijiji cha Umiru, Nyamninia, huku vyeti vyake vya masomo vikiwa vimewekwa kitandani kwake.
 

Uchunguzi wa polisi umebaini kuwa kabla ya marehemu kwenda kulala jana yake Januari 10, aliongea na mama yake kuhusu hali yake ya kukosa kazi.
 

Kwa mujibu wa polisi marehemu hakuacha ujumbe wowote bali aliacha tu vyeti vyake vyote kitandani. 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet