Mhudumu wa ndege aanguka na kufa mbele ya abiria
Eric Buyanza
January 4, 2024
Share :
Mhudumu wa ndani ya ndege ya British Airways alifariki baada ya kuanguka mbele ya abiria muda mfupi kabla ya ndege yao kuruka.
Kulingana na gazetili la Mail Online, msimamizi huyo mwenye umri wa miaka 52 alianguka ghafla wakati ndege hiyo ikijiandaa kuruka kutoka London kueleke Hongkong siku ya mkesha wa mwaka mpya.
Abiria waliokuwa na uzoefu wa mambo ya kitabibu wakishirikiana na madaktari waliofika baadae walikusanywa ili kujaribu kuokoa maisha ya mhudumu huyo lakini ilishindikana, huku safari ya ndege hiyo ikifutwa.
Janga hilo linaripotiwa siku chache baada ya msimamizi mwingine wa ndege ya shirika hilohilo la British Airways mwenye umri kama huo wa miaka 52, kufariki Desemba 23 akiwa Marekani.
Sababu rasmi ya vifo cha wahudumu wote wawili bado haijabainishwa.