Michael Carrick na rekodi mpya ndani ya Manchester United.
Joyce Shedrack
May 5, 2026
Share :
Kocha wa Manchester United Michael Carrick tangu alipochukua usukani, hakuna klabu nyingine katika Ligi Kuu ya Uingereza (Premier League) iliyokusanya alama nyingi kuliko Manchester United. Kabla ya Carrick kuanza kazi tarehe 13 Januari 2026, Manchester United ilikuwa chini ya Ruben Amorim.

Katika kipindi hicho, timu ilikuwa imecheza michezo 21 na kufanikiwa kukusanya jumla ya pointi 32 pekee. Wakati huo, United ilikuwa inasua-sua katika nafasi ya 7 kwenye msimamo wa ligi.
Tangu Carrick awe kocha, ameisimamia timu katika michezo 14 ya Premier League mpaka sasa (Mei 4, 2026). Katika michezo hiyo 14, ameshinda mechi 10, ametoa sare 2, na amepoteza mechi 2 pekee. Hii inamaanisha kuwa yeye mwenyewe amekusanya pointi 32 nyingine ndani ya muda mfupi sana.
Kwa sasa, ukijumlisha pointi 32 alizozikuta na pointi 32 alizozitafuta yeye, Manchester United ina jumla ya pointi 64 baada ya michezo 35.
Mafanikio haya yamewapandisha kutoka nafasi ya 7 mpaka nafasi ya 3, jambo ambalo limewahakikishia kurudi kwenye mashindano ya Champions League msimu ujao. Ni wazi kuwa Carrick amekusanya pointi sawa na zile zilizopatikana nusu nzima ya kwanza ya msimu, lakini yeye ametumia mechi chache zaidi kufanya hivyo.





