MICHAEL OWEN: Ni mapema mno kumfukuza Carrick Manchester United
Eric Buyanza
October 13, 2026
Share :

Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Manchester United, Michael Owen, ameitaka bodi ya klabu hiyo kutofanya maamuzi ya kukurupuka ya kumfukuza kocha Michael Carrick, akisisitiza kuwa anastahili kupewa muda wa kukua na kuijenga timu hiyo.
Licha ya mashabiki kueleza kutoridhishwa kwao kufuatia sare ya hivi karibuni ya 1-1 dhidi ya Tottenham Hotspur, Owen anaamini kuwa mabadiliko ya mara kwa mara ya makocha yamekuwa yakiiumiza klabu hiyo badala ya kuisaidia.
“Nadhani wanapaswa kumwacha akue. Bado ni kocha kijana, lakini tayari amethibitisha kuwa anaweza kupata matokeo makubwa mara kwa mara.
Ukiangalia yale aliyofanya msimu uliopita, nadhani ni vigumu kuhalalisha uamuzi wa kutafuta kocha mpya.”
Owen anaamini Carrick anastahili muda zaidi wa kujiendeleza badala ya United kuharakisha kumleta kocha mwingine.
Alikumbusha kuwa Manchester United tayari imeshapitia vipindi vya kujaribu makocha wa kila aina—kuanzia majina makubwa duniani kama Jose Mourinho na Louis van Gaal, hadi makocha vijana wenye mbinu mpya kama Ruben Amorim—lakini hakuna aliyedumu.
Kama shabiki wa Man United, unakubaliana na ushauri Owen?





