pmbet

"Michezo mingi ya Ligi Kuu Uingereza haivutii kuitazama" - Arne Slot

Eric Buyanza

March 2, 2026
Share :

Arne Slot anasema hawezi kusema anafurahia kutazama mechi nyingi za Ligi Kuu, lakini hatobadilisha mtindo wa uchezaji wa Liverpool.

 

Amesema anataka kuona timu yake inacheza mpira wa kuvutia na kushinda, si tu kutafuta matokeo.
 

"Ndio mtindo wetu, na nina uhakika tutaendelea kucheza hivyo," alisema Muholanzi huyo.

Kocha huyo aliyeipa Liverpool ubingwa wa ligi kuu msimu wake wa kwanza, amesema timu nyingi haziburudishi lakini unapata kuona ushindani unaoifanya ligi hiyo ya Uingereza ionekane ligi nzuri.

Michezo mingi ninayoiona kwenye Ligi Kuu si furaha kwangu kuitazama,” Slot alisema, “lakini huwa ya kuvutia kila wakati kwa sababu ina ushindani mkubwa na hiyo ndiyo inafanya ligi hii kuwa nzuri – kwa sababu kuna ushindani mwingi. Kila mtu anaweza kushinda dhidi ya mwenzake."
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet