Mido Man Utd kujiunga na Napoli ni suala la muda tu
Sisti Herman
August 26, 2024
Share :

Kiungo wa kati wa klabu ya Manchester United Scott McTominay amefikia makubaliano ya kujiunga na klabu ya Napoli ya ligi kuu nchini Italia kwa ada ya uham,isho ya Euro Milioni 30 (zaidi ya Tsh Bilioni 90).
Kiungo huyo raia wa Scotland ana asilimia kubwa za kujiunga na Napoli ndani ya wiki hii na tayari ameshaanza kuondolewa kwenye mipango ya Man Utd.