Miezi 20 ya Kocha Hemed, Taifa Stars imepiga hatua, hajawaangusha 'wazawa'
Sisti Herman
November 5, 2025
Share :

Jana Shirikisho la soka nchini (TFF) lilitangaza rasmi kusitisha mkataba na kocha mkuu wa timu ya Taifa Tanzania 'Taifa Stars' Hemed Suleman 'Morocco' kwa makubaliano ya pande mbili.
Kocha huyo aliyekaimu nafasi hiyo Januari 2024 kwenye michuano ya AFCON kutoka kwa kocha Adel Amrouche raia wa Algeria aliyesimamishwa na CAF na TFF kwa kutamka maneno yenye viashiria vya uchochezi wa kisiasa baina ya nchi za Algeria na Morocco.
Kwenye makala hii nimeandaa mambo niliyoyaona kipindi hichi timu ikiwa chini ya kocha Hemed;
1. KUPANDA KWENYE VIWANGO VYA UBORA VYA FIFA
Kwenye makala yangu niliyoandika tarehe 10 Oktoba 2024, nilieleza namna Taifa Stars ilivyopanga zaidi ya nafasi 10 kwenye viwango vya ubora vya shirikisho la soka duniani (FIFA) maarufu kama FIFA Rankings chini ya kocha Hemed ambapo aliichukua ikiwa nafasi ya 121 na kuisogeza had nafasi ya 110, soma zaidi hapa chini;
Gusa hapa kusoma zaidi; https://pmtv.co.tz/blog/fifa-rankings-tanzania-ilivyopanda-nafasi-10-ndani-ya-miezi-10
Hadi wakati huu anaiacha timu, anaiacha ikiwa nafasi ya 107, ikiwa imetoka kupanda hadi nafasi ya 103.
2. MBINU
Hizi ni taswira tofauti za mbinu za uchezaji wa Taifa Stars chini ya kocha Hemed;
(i) Aliboresha uzuiaji
Akiwa na Taifa Stars kocha Hemed aliboresha zaidi timu kimbinu kuwa bora kiuzuiaji kuliko ilivyokuwa mwanzo wakati anaichukua ambapo kwenye jumla ya michezo 30 aliyoiongoza, ilipata hati safi (Clean Sheets) 16, rekodi ambayo haikuwahi kuwepo mwanzo, mfano wa mbinu za timu yake kiuzuiaji zipo kwenye tathmini ya michezo hii niliyoichambua;
• Namna wanavyozuia kwenye nusu yao (Low & Mid Block)
- Video vs Morocco AFCON 2023; https://www.instagram.com/reel/C2NvUuUrvX6/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==
- Video vs Ethiopia WorldCup 2026 Qualifier; https://www.instagram.com/reel/C_v9twpq_sl/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==
- Analysis vs Morocco, World Cup 2025 Qualifiers; https://www.instagram.com/reel/DHqTOCFCeOJ/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==
• Namna wanavyozuia kwenye nusu ya mpinzani (High Pressing)
- Video vs Zambia World Cup 2026 Qualifiers; https://www.instagram.com/reel/C8Fjusgq_-e/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==
(ii) Matumizi ya mifumo/Miundo tofauti ya uchezaji
Stars chini ya kocha Hemed imecheza kwa kutumia mifumo tofauti, kulingana na aina ya wachezaji aliokuwa nao, mfano Mifumo yenye mnyumbuliko mkubwa wa viungo kwenye mechi mmoja kuanzia 4-2-3-1, 4-4-2 na 4-1-4-1, mfano rejea clip za mechi hizi hapo juu;
- vs Zambia
- vs Ethiopia
(iii) Wakishambulia (In Possession)
Licha ya kuwa na staili inayoelekeweka ya kucheza, mfano kwenye haya magoli:
- Video vs Guinea, AFCON 2025 Qualifiers; https://www.instagram.com/reel/DCj6N4fNKB1/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==
- Video vs Sudan, CHAN 2025 Qualifiers; https://www.instagram.com/reel/DB61Ks7tXYS/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==
Lakini, mapungufu ya wazi kwenye timu yake kiuchezaji yalikuwa pindi timu inapomiliki mpira, Mapungufu kama;
- Timu kutokuwa na wastani mzuri wa kumiliki mpira, ilishindwa kutawala wapinzani wengi kwasababu hii
- Timu kutokuwa na wastani mzuri wa kutengeneza nafasi za kufunga na hata kufunga magoli mengi.
- Timu kutokuwa na uwiano mzuri wa muundo wa kuweza kumeza mashambulizi ya kujibu, zaidi ya nusu ya magoli waliyofungwa yametokea sekunde 10 baada ya wao kuupoteza
(iv) Ubora kwenye mashambulizi ya kujibu
Licha ya kuwa kwao bora kiuzuiaji kuwapa Clean Sheet, lakini pia kupitia uzuiaji bora waliweza kupora mipira na kufanya mashambulizi ya kujibu yaliyowapa magoli, mfano;
• Uzuiaji mzuri zilisaidia timu kuweza kufanya mashambulizi ya kujibu kabla wapinzani hawajarejea kwenye muundo mzuri wa kuzuia (Offensive Transitions), mfano ni sehemu ya rejea za mechi pale juu dhidi ya:
- vs Zambia, uzuiaji mzuri uliweza kupora mpira na kuwapa goli 1 kupitia Offensive Transition
- vs Ethiopia uzuiaji mzuri uliweza kupora mpira na kuwapa goli 2 kupitia Offensive Transition
(v) Mapungufu ya kiuzuiaji kwenye mashambulizi ya kujibu (Difensive Transitions)
- Video vs Madagascar, COSAFA 2025; https://www.instagram.com/reel/DKnNwVci3nO/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==
- vs Ethiopia walifungwa goli 1
- vs DR Congo AFCON 2025 Qualifiers
(vi) Mapungufu kwenye mipira ya kutenga (Set Plays)
- Analysis vs DR Congo, AFCON 2025 Qualifiers; https://www.instagram.com/p/DBJ3BwYtKGs/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==
3. KUSOMA WAPINZANI ILIKUA SILAHA YAKE
Kwenye makala niliyoiandika June 14 2025, nilieleza namna Kocha Hemed anavyotumia silaha muhimu vitani ya kumjua unayeenda kucheza naye (Opposition Analysis)
Soma hapa; https://www.instagram.com/reel/DK41dICiE6y/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==
Kwenye benchi lake la ufundi alikuwa na watu makini kwenye jukumu hilo kama Gabriel Jonson, mtathmini wa viwango wa Taifa Stars anamsaidia kufanya kazi hizo
4. HATUA KUBWA ZAIDI CHAN 2025
Kwa Mara ya kwanza kwenye historia, kocha Hemed aliiongoza Tanzania kwenye michuano mikubwa ya Afrika ambapo aliisaidia kufika robo fainali ya michuano ya CHAN 2025 akiisiadia kushinda mechi 3, sare 1 na kupoteza mchezo 1
Hizi ni tathmini ya kimbinu za michezo yote ya Taifa Stars CHAN 2025;
• Tanzania 1-0 Burkina Faso;
- Analysis; https://www.instagram.com/reel/DM5sjF1ig6j/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==
- POTM; https://www.instagram.com/p/DM3UipUtbGu/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==
• Mauritania 0-1 Tanzania
- Analysis; https://www.instagram.com/reel/DNDl7HXCEC4/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==
- POTM; https://www.instagram.com/p/DNBpmkZNLXg/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==
• Tanzania 1-2 Madagascar
- Analysis; https://www.instagram.com/reel/DNLs2yRiwYE/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==
- POTM; https://www.instagram.com/p/DNJfvagti4k/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==
• Morocco 1-0 Tanzania
- Analysis; https://www.instagram.com/reel/DNruCm-0MN4/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==
• Overall CHAN 2025 Analysis; https://www.instagram.com/reel/DNwCdt8xI42/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==
5. UITWAJI WA KIKOSI MECHI ZAKE ZA MWISHO (Squad Selection)
Mechi za 3 za mwisho baada ya CHAN, Taifa Stars chinj ya kocha Hemed ilipoteza michezo yote, pengine inaweza kuwa sababu ya kusitishiwa mkataba.
Wengi wameonyesha kutokuwa na Imani na aina ya kikosi ambacho huwa wanakiita Mara kwa mara
Kwenye mechi hizo 3 za mwisho nilitoa tathmini yangu kabla ya michezo kuhusu uitwaji wake wa kikosi, hii hapa chini
Video; https://www.instagram.com/reel/DOGwXEIgt2X/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==
Taifa Stars ilipoteza mechi hizo zote 3, huku mechi 2 zikiwa za kuwania kufuzu Kombe la dunia 2026 ambazo pia nilizifanyia tathmini;
- Video vs Niger, World Cup 2026 Qualifiers: https://www.instagram.com/reel/DOY1PTSAhnR/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==
-Video vs Zambia, World Cup 2026 Qualifiers: https://www.instagram.com/reel/DPkLWfpggYm/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==
Mechi ya mwisho ya Taifa Stars chini ya kocha Hemed ikawa ya kirafiki dhidi ya timu ya Taifa Iran, hii pia niliifanyia tathmini;
- Video, Match; https://www.instagram.com/p/DPzOCRUDUW8/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==
- Video, Studio; https://www.instagram.com/reel/DP1NN8tghv5/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==
Kila la kheri Kocha Hemed, chini yako Tanzania imepiga hatua kwenye mchezo wa soka.





