Mihogo na viazi vitamu vimenisaidia kupunguza uzito kilo 30 - Museveni
Eric Buyanza
March 25, 2026
Share :

Lishe ya mihogo, viazi vitamu na mboga za asili imemsaidia Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, kupunguza kilo 30, ameiambia BBC.
“Afya yangu imekuwa nzuri kila wakati, lakini madaktari walifanya makosa na kisha nikaamua kupunguza uzito,” alisema Bw. Museveni.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 75 awali hakuwa na ufahamu wa uzito wake, ambao ulikuwa ni kilo 106.
Alikanusha maoni kwenye mitandao ya kijamii kwamba “anaonekana mchovu,” akisema amepunguza uzito kidogo tu.
Alisema kwenye blogu yake ya kibinafsi mwezi uliopita: “Nimekwepa kuwa na mwili mnene, kwa sababu madaktari hawakunielezea kuwa hii inasababisha matatizo au kwamba ni lazima kukabiliana na unene kupita kiasi.”
Aliongeza kuwa uzito wake wa sasa ni kilo 76, unaolingana na urefu wake wa futi 5 na inchi 7 (170cm).
Hata hivyo, Bw. Museveni hakueleza ni muda gani uliochukua kupunguza kilo 30.
“Ninakula mizizi ya mihogo kwa sababu sili chakula chenu cha Ulaya au Asia. Ninakula chakula chetu kama; mihogo, ndizi, viazi na mboga zetu za asili,” alisema Bw. Museveni kwa BBC.





