pmbet

Miili 21 yaopolewa katika ajali ya Boti

Eric Buyanza

April 24, 2024
Share :

Watu kadhaa wamepoteza maisha baada ya boti iliyokuwa imebeba wahamiaji kuzama kwenye pwani ya Djibouti, shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa lilisema jana.
 

Ilikuwa ajali ya pili mbaya ya baharini ndani ya wiki mbili kutoka kwenye taifa hilo ambalo liko kwenye ile inayoitwa Njia ya Uhamiaji ya Mashariki kutoka Afrika hadi Mashariki ya Kati.
 

Meli nyingine iliyokuwa imebeba wahamiaji wengi wa Ethiopia ilizama katika eneo hilo hilo Aprili 8, na kupoteza maisha ya watu kadhaa.
 

Mkuu wa ujumbe wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji nchini Djibouti, Tanja Pacifico, ameliambia shirika la habari la AFP mjini Nairobi kwamba miili 21 imepatikana, huku watu 23 wakiwa bado hawajapatikana.
 

Watu wengine 33 walinusurika kwenye janga hilo, alisema Jumanne usiku.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet