Miili 6 ya watu na bodaboda 6 zatolewa eneo la ajali Kimara.
Joyce Shedrack
February 14, 2025
Share :
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni RPC Mtatiro Kitinkwi amethibitisha kuwa bodaboda sita zimetolewa chini ya lori ambalo liliacha njia na kuparamia abiria na madereva wa bodaboda katika eneo la Kimara Stop Over jijini Dar es Salaam.

Taarifa ya awali iliyothibitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Albert Chalamila ilieleza kuwa miili ya watu watatu ilitolewa chini ya lori hilo hadi kufikia saa 9:00 Usiku wakati zoezi la uokoaji likiendelea.
Zoezi la kuliondoa lori hilo lenye namba za usajili T 908 BYM limeendelea ambapo kwa mujibu wa RC Chalamila hadi kufika saa 9 Usiku lilinyanyuliwa kwa zaidi ya asilimia 95%.





