pmbet

Miili 60 yapatikana baada ya Operesheni ya Israel

Eric Buyanza

July 12, 2024
Share :

Maafisa katika eneo linalodhibitiwa na Hamas wamesema takriban miili 60 imepatikana kwenye vifusi katika viunga vya mji wa Gaza. Hii baada ya jeshi la Israel kutangaza kusitisha operesheni yake katika eneo hilo.
 

Israel ilirusha makombora katika mji wa Gaza kwa wiki moja mfulizo, hatua ambayo wakazi wameitaja kama vita vikali zaidi tangu mashambulizi yalipoanza.
 

Miili hiyo 60 imepatikana baada ya wanajeshi wa Israel kumaliza operesheni ya wiki mbili ambayo Jeshi la Ulinzi la Raia la Gaza na wakaazi wanasema imeacha eneo hilo kuwa magofu.
 

Msemaji wa Ulinzi wa Raia Mahmud Bassal amesema asilimia 85 ya majengo yameharibiwa na kulitaja eneo la Shujaiya kama "eneo la maafa".
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet