Miili ya Askari watano waliofariki kwa ajali yaagwa Singida.
Joyce Shedrack
September 22, 2026
Share :
Miili ya askari watano wa Jeshi la Polisi Tanzania waliofariki dunia katika ajali ya barabarani iliyotokea Septemba 21, 2026, eneo la Sekenke mkoani Singida, imeagwa leo Septemba 22, 2026, katika Viwanja vya Shule ya Msingi Shelui, Wilaya ya Iramba mkoani Singida.

Zoezi la kuaga miili hiyo limehudhuriwa na viongozi wa mbalimbali wa Jeshi la Polisi, viongozi wa serikali, viongozi wa Taasisi za Kidini, Maafisa wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na wananchi wa Mkoa wa Singida, likiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego.
Viongozi mbalimbali wameendelea kutoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na Jeshi la Polisi Tanzania kufuatia msiba huo, huku wakitambua mchango wa askari hao katika kulinda usalama wa wananchi na mali zao.
Jeshi la Polisi Tanzania linaendelea kutoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, askari na Watanzania wote walioguswa na msiba huo, na kuwaombea marehemu wapumzike kwa amani.





