Mikel Arteta aweka akili yote kwa Msweden, Alexander Isak
Eric Buyanza
May 4, 2024
Share :
Meneja wa Arsenal Mikel Arteta anaelezwa kuweka kipaumbele kikubwa kwenye kuisaka huduma ya mshambuliaji wa Newcastle na timu ya taifa ya Sweden, Alexander Isak.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 amekuwa akihusishwa kwa muda sasa kuhamia Emirates Stadium.
Isak, ambaye mkataba wake unamalizika 2028, amecheza mechi 26 za Ligi Kuu msimu huu, akifunga mabao 19.
Aina ya uchezaji wake umeripotiwa kuvutia baadhi ya vilabu vikubwa barani Ulaya.