Mila inayomtaka shangazi wa Bibi Harusi kushiriki mapenzi na Bwana Harusi
Eric Buyanza
January 15, 2024
Share :
Watu wa kabila la Banyankole ni kundi la kuhamahama (wafugaji) ambalo linaishi katika baadhi ya maeneo ya Magharibi mwa Uganda. Kundi hili la watu lilifuata desturi ya kipekee ya ndoa iliyoanzia karne ya 15 katika Ufalme wa Kibantu wa Ankole nchini humo.
Kwa miaka mingi, kabila la Banyankole lilikuwa na majukumu ya kipekee kwa shangazi hasa siku ya harusi ya mpwa wake.
Desturi hiyo ijapokuwa imepitwa na wakati, ilikuwa ni ile iliyomtaka shangazi wa bibi harusi kufanya ngono na Bwana harusi ili kupima uwezo na nguvu za Bwana harusi.
Kando na kulala na Bwana harusi, shangazi pia alilazimika kuthibitisha kama Bibi harusi amehifadhi ubikira wake vizuri kabla ya ndoa.
Ni pale tu ambapo ubikira ulipothibitishwa ndipo ndoa hiyo ingeruhusiwa kufungwa.