'Milionea Kibu Denis' aikamua Al Nasser zaidi ya Tsh bil. 1.8
Sisti Herman
February 12, 2026
Share :

'Milionea Kibu Denis' ndiyo vamna mpya anayoweza kuitwa nyota huyo aliyeondoka Simba SC kujiunga na Al Nasser ya Libya.
Kwa mujibu wa Mwandishi wa habari mwandamizi @charlesabel24, Kibu Denis atavuna kiasi cha Dola 700,000 (zaidi ya Tsh Bilioni 1.8) katika mkataba wake wa mwaka mmoja na nusu na Al Nasser ya Libya.
Nusu ya fedha hizo, Dola 350,000 (Zaidi ya Tsh Millioni 900) ataingiziwa katika akaunti yake moja kwa moja kama dau la ushawishi wa kusaini mkataba.
Nusu iliyobakia ambayo ni Dola 350,000 (zaidi ya Tsh Milioni 900) atakuwa akilipwa kila mwezi kama mshahara na bonasi ambapo kwa mwezi atakuwa akipokea Shilingi milioni 50 za Kitanzania.
Mwanahabari huyo pia ameeleza kuwa leo Kibu Denis atasafiri na meneja wake @carlos_mastermind kwenda Libya kukamilisha uhamisho huo.





