pmbet

Milioni 25 zapatikana, ndani ya siku 7 za kumchangia Lissu gari

Eric Buyanza

May 27, 2024
Share :

Michango ya fedha kutoka kwa wafuasi na wanachama wa CHADEMA kwa ajili ya kumnunulia gari Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu umefikia Sh. milioni 24.9 ndani ya siku saba tangu kuanzishwa kwa harambee hiyo. 

Lissu alithibitisha kupokea kiasi hicho cha fedha kupitia mtandao wake wa X (zamani Twitter) juzi na kuomba wadau waendelee kumchangia apate gari hilo "kwa ajili ya harakati za ukombozi".

Mei 17 mwaka huu, wafuasi wa mwanasiasa huyo wakiongozwa na Mwanaharaki Maria Sarungi, waliazimia kumchangia fedha mwanasiasa huyo anunue gari jipya ili lile la zamani ambalo lilishambuliwa kwa risasi lihifadhiwe kwa ajili ya ukumbusho.

"Tumekamilisha wiki moja ya mchango. Hadi sasa tumepokea Sh. 24,956,282.00 kutoka kwa wachangiaji 2,243. Kwa wastani, kila siku wachangiaji 320 wametoa Sh. 11,126.30 kila mmoja," aliandika Lissu kwenye ukurasa wake wa X.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet