Milioni 250 zatengwa kwa vijana 20 wenye mawazo bunifu
Eric Buyanza
March 16, 2024
Share :
Jumla ya Sh milioni 250 zimetengwa kwa vijana 20 watakaoshinda wazo la ubunifu kuhusu changamoto ya ufanisi katika nishati nchini lengo likiwa ni kuimarisha mazingira ya matumizi bora kwa kukuza ubunifu na uvumbuzi.
Hayo yameelezwa jana Machi 15, 2024 jijini Dodoma na Afisa Mawasiliano kutoka Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP), Jolson Masaki wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa kutatua changamoto ya ubunifu kwa ufanisi wa nishati.
Mpango huo ni kwa kushirikiana kati ya Wizara ya Nishati, Umoja wa Ulaya (EU), Ubalozi wa Ireland na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Masaki amesema Mpango huo unaungwa mkono na hazina kubwa ya Sh milioni 250 za Kitanzania na unafanywa ili kuimarisha mazingira ya matumizi bora ya nishati kwa kukuza ubunifu na uvumbuzi.