pmbet

Milipuko mikubwa jijini Nairobi, 2 wafa, 222 wakijeruhiwa

Eric Buyanza

February 2, 2024
Share :

Watu wawili waripotiwa kufa na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa kwenye mtaa wa Embakasi, mjini Nairobi baada ya mtambo wa gesi kulipuka usiku wa kuamkia leo na kuwaweka wakazi wa jiji hilo kwenye hofu kubwa, gazeti la Daily Nation linaripoti.
 

"Milipuko mikubwa ilisikika, huku watu wakipiga kelele na kukimbia hovyo kujaribu kukoa maisha yao,” alisema mmoja wa mashuhuda.
 

Moto huo umeteketeza majengo jirani, huku wakazi wa makazi jirani kama vile Nyayo Embakasi wakitoka majumbani mwao kwa wingi huku wakipiga kelele za hofu.
 

Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya na kikosi cha zima moto walikuwa wanaendelea kupambana na moto huo saa kadhaa baada ya mlipuko huo.
 

Msemaji wa serikali Isaac Mwaura amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mlipuko huo ulitoka kwenye kiwanda cha gesi kilichopo kwenye eneo la makazi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet