pmbet

Mimi na mke wangu tunapumzika kuzaa - Davido

Eric Buyanza

April 21, 2025
Share :

Kutoka nchini Nigeria, msanii wa muziki wa Afrobeats, Davido, ameweka wazi kuwa yeye na mke wake Chioma, wanapumzika kuzaa.

Davido anasema hayuko tayari kuendelea kuzaa kwasasa, akisisitiza kuwa ni wakati sahihi wa mke wake kupata mapumziko ili aweze kufanya mambo yake mengine.

"Sitaki watoto zaidi sasa. Mimi na mke wangu tunapumzika. Anahitaji kutoka kwenda kazini. Anataka kufanya mambo mengi kama vile kufungua mgahawa wake na kuzindua viungo vyake. Ninahisi anastahili mapumziko ya miaka kadhaa baada ya kupata watoto 3." alisema Davido

Itakumbukwa wawili hawa mwaka 2023 walikaribisha mapacha, ikiwa ni mwaka mmoja kupita tangu kumpoteza mtoto wao wa kwanza aliyefariki kwa kutumbukia kwenye bwawa la kuogelea.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet