Mimi na P-Funk tulitengeneza Bongo Fleva kwa kuchanganya Zouk, Reggae..
Eric Buyanza
December 27, 2023
Share :
Mtayarishaji mkongwe wa muziki Master J amewataka watayarishaji wa muziki na wasanii wa sasa kuwa wabunifu zaidi ili muziki wa Tanzania uweze kwenda mbali zaidi kuliko sasa ambavyo umeishia kuwa bora Afrika mashariki pekee.
"Mimi nimeshastaafu kutayarisha muziki, wasanii na watayarishaji wa sasa wanahitajika kuwa wabunifu sana ikiwemo kutengeneza utambulisho wa muziki wetu, mimi na P-Funk tulitengeneza Bongo Fleva kwa kuchanganya Zouk, Reggae na mengine, wasanii sasa wanapaswa kuitengeneza identity yetu" anasema Master J.
"Asake ametoboa baada ya kuchanganya Amapiano na Afro Beats, hata sisi tuna ile Singeli ikichanganywa na Amapiano au afro Beats unaweza kupata ladha tofauti"
“Hauwezi kushindana na kushinda Grammy kama huna identity, lazima utashindwa na wenye identity zao, msanii wa Tanzania hawezi kuimba vizuri Amapiano kuliko wa Afrika kusini au Afro Beats kuliko wa Afrika magharibi”.