"Mimi ndiye mshiriki mzee zaidi wa Miss Universe nikiwa na miaka 60" - Alejandra
Eric Buyanza
April 27, 2024
Share :
Mwanamke mmoja wa Argentina aliyefahamika kwa jina la Alejandra Rodriquez, amekuwa mshiriki mzee zaidi wa (Miss Universe) akiwa na umri wa miaka 60.
Habari za Alejandra zimekuwa gumzo ulimwenguni kote na kwenye mitandao ya kijamiii.
Hapo awali, umri wa washiriki wa Miss Universe ulitakiwa kuwa kati ya miaka 18 hadi 28 na kigezo kingine ilitakiwa (usiwe na mtoto) lakini sheria hizo zilibadilishwa mwaka jana.
Pamoja na uzee wake mwanamke huyo bado anageuza vichwa na shingo za wanaume wengi kutokana na mwonekano wake mzuri.
Mwenyewe anasema haya;
"Jambo la msingi ni kuwa na maisha yenye afya, kula vizuri, kufanya mazoezi ya viungo, hakuna kitu kingine cha ajabu" aliuambia mtandao wa El Trece.
Alejandra Rodriquez anasema yeye hufuata lishe yake ipasavyo, ambayo inajumuisha ulaji bora na kufunga mara kwa mara.