"Mimi ni mkali kwenye uandikaji wa mashairi" - Marioo
Eric Buyanza
December 30, 2023
Share :
Msanii kunako muziki Bongofleva, Omar Mwanga 'Marioo' amesema yeye ni mzuri kwenye utunzi wa nyimbo nzuri na ndio maana amekuwa bora kwenye kazi zake.
Mario anasema kabla ya mambo ya kushindana kwenye kutumia gharama kubwa kwa ajili ya kuandaa vichupa vikali (video), yeye alikuwa ni muumini wa audio kali.
“Video kali inatokana na mashairi mazuri ya wimbo, huwezi kuwa na wimbo mbaya ukabebwa na video, sijisifu, mimi ni bora kwenye mambo ya kuandika mashairi mazuri angalia nyimbo zangu hata nilizowaandikia baadhi ya wasanii ni kubwa;
“Hivyo naamini katika uandishi mzuri wa mashairi kabla ya kufikiria nitafanya video ya aina gani hasa kipindi hiki ambacho tumekuwa waumini wa kutumia gharama kubwa kuhakikisha tunatengeneza video kali,” alisema.
NMG