pmbet

Minziro atua Fountain Gates kuikabili Simba April 15.

Joyce Shedrack

April 10, 2026
Share :

Klabu ya Fountain Gate FC imetangaza rasmi uteuzi wa Fred Felix Minziro kuwa Kocha Mkuu mpya wa timu hiyo.

Minziro ataongoza benchi la ufundi akisaidiwa na makocha wasaidizi Mathias Wandiba na Abubakari Ally Francis, ambao wataendelea na majukumu yao ndani ya klabu.
No photo description available.
Uongozi wa klabu umeeleza kuwa una imani kubwa na uzoefu wa Minziro, ukiamini kuwa ataleta mabadiliko chanya, kuimarisha ushindani na kusaidia timu kufikia malengo yake ya kimashindano.

Katika hatua nyingine, klabu hiyo imethibitisha kuachana na aliyekuwa Kocha Mkuu, Mohamed Laizer, kwa makubaliano ya pande zote, huku ikimshukuru kwa mchango wake katika kipindi chote alichohudumu.

Fountain Gate FC imemtakia kila la heri Kocha Laizer katika majukumu yake yajayo, huku ikiweka wazi dhamira ya kuendelea kujenga timu imara na yenye ushindani mkubwa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet