Misri kukipiga Argentina hatua ya 16
Eric Buyanza
July 4, 2026
Share :
Misri itakutana na Argentina katika hatua ya 16 Bora ya michuano ya Kombe la Dunia la FIFA 2026.Mtanange huo wa kihistoria umethibitishwa baada ya timu zote mbili kufanya vizuri katika mechi zao za hatua ya 32 bora.
Misri (Mafarao) walifanikiwa kutinga hatua hii kwa kuiondoa Australia kwa mikwaju ya penalti 4-2, baada ya mchezo wa dakika 90 na muda wa ziada kuisha kwa sare ya 1-1.
Argentina (Mabingwa watetezi) walipata ushindi mgumu wa mabao 3-2 dhidi ya Cape Verde katika mchezo uliomalizika kwenye muda wa nyongeza.
Misri imekuwa nchi ya tano barani Afrika kufuzu kutoka hatua ya mtoano, baada ya Cameroon (1990), Senegal (2002), Ghana (2010) na Morocco (2022 na 2026).






