pmbet

Misri mguu ndani mguu nje Afcon, Kumkosa Salah

Sisti Herman

January 19, 2024
Share :

Timu ya taifa ya Misri jana wamelazimishwa sare ya pili mfululizo na Ghana kwenye mchezo wa raundi ya pili hatua ya makundi ya kombe la mataifa Afrika (AFCON) kundi B, baada ya mchezo kumalizika kwa goli 2-2  katika dimba la Félix Houphouët-Boigny, Abidjan huku nyota wao Mohamed Salah akiumia nyama za paja sekunde kadhaa kabla ya mapumziko.

Magoli ya Ghana yote mawuili kwenye mchezo huo yalifungwa na Mohamed Kudus huku yale ya Misri yakifungwa na Mostafa Mohamed na Omar Marmoush.
 

Baada ya matokeo hayo, kundi B linaendelea kuongozwa na Cape Verde wenye alama 3 wakifuatiwa na Misri wenye alama 2 huku Msumbiji na Ghana wakiburuza mkia wa kundi kwa alama 1 kila moja wakitofautiana kwa idadi ya mabao ya kifunga na kufungwa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet