pmbet

Misri yaponea chupuchupu kupata fedheha AFCON

Eric Buyanza

January 15, 2024
Share :

Mkwaju wa penati uliopigwa na mshambuliaji Mohammed Salah katika dakika za majeruhi ndiyo uliowaokoa timu ya taifa ya Misri (The Pharaohs) kutoka kwenye fedheha kwenye mchezo wake wa kwanza wa michuano ya mataifa ya Afrika, AFCON, dhidi ya Msumbiji uliomalizika kwa sare ya bao 2-2 kwenye mchezo huo wa kundi B.
 

Penati hiyo ilitolewa baada ya kiungo Mostafa Mohamed kuchezewa madhambi, na Salah akapachika wavuni mkwaju ulioinyima Msumbiji ushindi wa kwanza wa kihistoria kwenye michuano hiyo ya kandanda barani Afrika.

Kwenye mchezo mwingine wa kundi B, timu ya soka ya Ghana ilikubali adhabu ya kipigo cha bao 2-1 kutoka kwa Cape Verde.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet