Miss World atoka Ulaya, Miss Tanzania aingia Top 10
Sisti Herman
March 10, 2024
Share :
Mwanadada Krystyna Pyszkován kutoka nchini Czech Republic ameshinda taji la Miss World 2024.
Moja ya vitu vilivyompa ushindi ni story yake ya Beauty with purpose ambayo ameitengenezea makala ya kusisimua iliyoanzia Nchini Tanzania akielezea jinsi alivyofanikisha kuanzishwa kwa Shule moja Jijini Arusha kwa kushirikiana na Sonta Foundation July mwaka 2022.
Fainali ya mashindano imefanyika jioni ya leo Machi 9, 2024 katika Jiji la Mumbai nchini India yalikokuwa yakifanyika mashindano hayo.
India iliandaa shindano la 71 ambapo washiriki kutoka nchi 115 walikuwa wakichuana kila mmoja akiwa na ndoto ya kurudi na taji hilo nchini mwake.
Miss Tanzania 2022, Halima Kopwe alikuwa miongoni mwa washiriki wa shindano hilo ambapo alitinga kumi bora katika kipengele cha ‘Beauty with Purpose Project’.
Taji hilo mwaka jana Miss World 2022 lilienda kwa Karolina Bielawska wa Poland ambaye mrithi wake Krystyna Pyszková amepatikana leo.
Waliomaliza 'top four' 1. Krystyna Pyszková wa Jamhuri ya Czech 2. Yasmina Zaytoun wa Lebanon 3. Aché Abrahams wa Trinidad 4. Lesego Chombo wa Botswana.