Mitandao ya kijamii yampa tuzo Cardi B ashinda Tuzo ya 160.
Joyce Shedrack
June 22, 2024
Share :
Rapa wa kike kutoka Nchi Marekani Cardi B ameshinda tuzo ya muhamasishaji bora mitandaoni siku ya jana katika usiku wa tuzo za ‘Hollywood Unlocked Impact Awards’ katika Hoteli ya Beverly Hilton nchini Marekani.
Cardi ameshinda tuzo hiyo baada ya kuonekana kuwa mwanamuziki mashuhuri anayeongoza kuwa na ushawishi kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii Duniani kote.
Hii inakuwa tuzo yake ya 160 tangu aanze sanaa ya muziki akiwa ni miongoni mwa wasanii wa Marekani wenye historia ya kusinda tuzo nyingi ikiwemo tuzo ya Grammy, miongoni mwa tuzo alizowahi kushinda Cardi B ni tuzo ya Grammy, tuzo 8 za Billboard Music Awards, tuzo 6 za Guinness World Records, tuzo 6 za American Music Awards, tuzo 14 za BET Hip Hop Awards, na tuzo mbili za ASCAP mwandishi bora wa mwaka zote akishinda kwa miaka tofautitofauti.