Mjadala wa mapadri kuruhusiwa kuoa waibuka tena
Eric Buyanza
January 10, 2024
Share :
Askofu Mkuu Charles Scicluna wa Malta, amesma kanisa linapaswa kufikiria sana kuhusu haja ya kuwaruhusu mapadri kuoa.
Akiongea kwenye mahojiano na gazeti la Times of Malta ambayo yaliyochapishwa Jumapili ya juzi, Charles Scicluna anasema.....
“Pengine ni mara ya kwanza ninayasema hadharani na matamshi yangu yataonekana kuwa ya uzushi kwa baadhi ya watu,” alisema Charles Scicluna.
“Kama ningekuwa na uwezo, ningerekebisha sheria ya kwamba mapadri/makasisi wanapaswa kubaki waseja.......Hili ni jambo tunahitaji kufikiria upya,”
Scicluna anasema Kanisa “limepoteza mapadri/makasisi wengi wazuri kwa sababu walichagua ndoa”.
Papa Francis amefutilia mbali uwezekano wowote wa kubadilisha sheria ya Kanisa Katoliki inayowalazimu mapadri kuishi bila kuoa.
Mjadala kuhusu iwapo makasisi wa Kikatoliki waruhusiwe kuoa umekuwepo kwa karne nyingi sasa.