pmbet

Mjasiriamali mdogo ajinyonga baada ya kukosa rejesho la mkopo

Eric Buyanza

April 26, 2024
Share :

Huko mkoani Dodoma mjasiriamali mdogo aliyefahamika kwa jina la Alfyo Chibwete mkazi wa mtaa wa Mpamaa, amefariki dunia kwa kujinyonga baada ya kushindwa kupeleka rejesho la mkopo (shilingi 49,000). 

Inaelezwa kuwa Chibwete alikuwa anapaswa kupeleka rejesho kila Jumanne sehemu aliyokuwa amekopa mkopo wa shilingi Milioni moja na laki mbili, ambapo hadi anakwenda kujinyonga deni lilikuwa limebakia shilingi 245,000.

Mke wa marehemu aitwae Martha amesema mume wake baada ya kukosa kiasi hicho cha rejesho la mkopo alituma ujumbe ukisema "Mama tunza wanangu mimi naenda kujinyonga"

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet