Mjerumani alyeshinda Ballon D'or na Kombe la Dunia afariki dunia
Sisti Herman
January 9, 2024
Share :
Mkongwe wa soka nchini Ujerumani Franz Beckenbauer mwenye umri wa miaka 78 anayetambulika kama moja ya wachezaji bora kuwahi kutokea nchini humo, amefariki dunia.
Franz aliwahi kucheza katika klabu ya BayernMunich mechi 582 na kufikia kiwango cha juu kama mchezaji na Meneja. Pia aliwahi kushinda ubingwa wa Ulaya mwaka 1972 akiwa kama mchezaji, vilevile alishinda Ballon d’OR mara mbili.
Mwaka 1974 alishinda Kombe la Dunia akiwa nahodha wa West Germany na mwaka 1990 alinyanyua tena kombe hilo akiwa Meneja.